Aliwahi
kucheza kwenye ligi ya England kwa muda wa miaka mitano akicheza kwenye
klabu ya Aston Villa kabla ya kujiunga na VFL Stutgart ya nyumbani kwao
Ujerumani ambayo aliisaidia kutwaa ubingwa wa ligi ya Ujerumani
Bundesliga.
Thomas
pia aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani kwenye mashindano ya
kombe la dunia na kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2008 ambako alicheza
mechi zote za hatua ya mtoano kuanzia robo fainali, nusu fainali na
fainali.
Moja ya vitu ambavyo Hitzlsperger atakumbukwa navyo
ni mashuti makali aliyokuwa anapiga kwa mguu wake wa kushoto na
alifunga mabao mengi sana kwa style hiyo kabla ya kustaafu soka mwaka
2013 akiwa na umri wa miaka 31 baada ya kuandamwa na majeraha tofauti ya
goti kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment