Mashindano ya Miss
East Africa mwaka huu yataonyeshwa LIVE kupitia Mnet ambapo yanatarajiwa
kutuizamwa na watu wanaokadiliwa kufikia million 200 kupitia televison
na kwa njia ya internet Dunia nzima.
Aidha maandalizi
ya mashindano hayo yanaendelea kwa kasi ambapo yamepangwa kufanyika
tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dare s
salaam, Tanzania badala ya mwezi September kama ilivyokuwa imetangazwa
awali ili kutoa muda zaidi kwa Ncgi ambazo hazijapata wawakilishi wao
kuweza kukamilisha zoezi hilo.
Mashindano ya Miss
East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake ambapo
yatashirikisha warembo kutoka katika Nchi 16 za ukanda wa afrika
mashariki.
Nchi
zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja
na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja
na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
Mashindano ya Miss
East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa
Afrika mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi
wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika
Tayari baadhi ya
Nchi zinazoshiriki mashindano hayo zimeshatangaza wawakilishi wake
ambazo ni Eritrea, Ethiopia, Uganda, Southern Sudan, Malawi na
Seychelles. Nchi zilizosalia zinatarajiwa kutangaza wawakilishi wao
kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni tarehe 28 mwezi September.
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.
Rena Callist,
Executive Producer,
MISS EAST AFRICA PAGEANT
No comments:
Post a Comment