MWANAMITINDO maarufu nchini, Jack Patrick amemtetea msanii Juma Khalid
‘Jux’ kwa kusema ni marafiki wa kawaida na kukanusha taarifa za uhusiano wa
kimapenzi zilizozagaa.
*Jack akiwa na Jux katika pozi.*
Alisema anapoona katika mitandao na baadhi ya magazeti yakiandika kuhusu
uhusiano wa kimapenzi, hujisikia vibaya kwa vile kunamtibulia kwa mpenzi
wake anayemhisi vibaya.“Kama kuna mapenzi lazima ningeweka wazi tu na kama
itatokea nitaweka wazi, naomba watu wasinihukumu kwa kutumia picha, picha
ni nyingi na wataona nyingi zikiendelea kwa sababu sisi wote tunapenda
kupiga picha,”
No comments:
Post a Comment