Kampeni
za uchaguzi zimemalizika nchini Angola huku wananchi wakitarajiwa
kushiriki uchaguzi wa bunge hii leo Ijumaa, majira ya saa moja kwa saa
za Angola.
Ushindani
mkali unatarajiwa kuwa kati ya chama tawala MPLA na kile cha upinzani
UNITA. Hata hivyo, wachambuzi wa kisiasa wanatabiri kuwa chama tawala
huenda kikajipatia ushindi mkubwa kutokana na serikali ya Rais Edwardo
Dos Santos kutumia raslimali nyingi za serikali kwenye kampeni zake.
Wakati huo huo kiongozi wa chama cha UNITA, Isaias Samakuva amedai kuwa
maisha yake yako hatarini. Duru za karibu na mwanasiasa huyo zinasema
kuwa, mtu mwenye silaha alikamatwa juzi katika mkutano wa kisiasa
alipokuwa akimkaribia Bw. Samakuva. Serikali imekanusha kuhusika na
tukio hilo na imeahidi kumuongezea ulinzi mkuu huyo wa upinzani.
No comments:
Post a Comment