• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, June 21, 2012

    Wema Sepetu: "Kila mtu atasema lake, there is time tuache mengine yapite"



    Baada ya jana na juzi habari za Wema Sepetu kudanganya umiliki wa nyumba yake kusambaa kwa kasi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, mrembo huyo ameibuka na kusema ‘inatosha.’
    Inadaiwa kuwa nyumba ya muigizaji huyo aliyodai kuwa ameijenga kwa fedha yake mwenyewe na kutumia karibu milioni 400 mpaka inakamilika sio ya kwake kama alivyosema.
    Jana kupitia mtandao wa Twitter aliandika, “ Kila mtu atasema lake, there time tuache mengine yapite.”
    Katika hatua nyingine jana mama yake mzazi amesema amechoka na habari zinazozushwa dhidi ya mwanae kwenye magazeti ya udaku na ameapa kumpeleka mtu mahakamani kwa kuharibu jina la Wema.
    Amesema kuwa alichokigundua ni kuwa binti yake hana rafiki wa kweli.
     Akiongea na kipindi cha Take One cha Clouds jana usiku, mama huyo amesema kuna watu wamemfanya afanye mambo ambayo hakutegemea kama angeyafanya katika maisha yake.
    Mambo hayo ni pamoja na kumpeleka Wema kwa waganga ili atengenezwe na sasa mwanae yuko fit japokuwa anasema alihangaika sana.
    “Mama Wema kafunguka kama geti la milango miwili, kavunja hadi fensi hakuna siri tena,hadi kwa waganga duuu!” alitweet mmoja wa watu waliokuwa wakiangalia kipindi hicho.
    “Mama yako kakutetea vizuri sanaa @wema_sepetu, usimvue nguo tena, achana na marafiki wa mjini, concentrate na mambo yako! Mfanye mama yako ndo msiri wako, hakuna urafiki kwenye maisha ya sasa!” aliandika mwingine.
     Katika hatua nyingine mtangazaji wa kipindi hicho, Zamaradi Mketema amejikuta lawamani kutokana na kashfa hiyo ya Wema kudanganya kwenye kipindi chake.
    “Mimi mwandishi, unapokwenda kufanya interview na mtu ninachotakiwa kusikiliza ni kile ninachoambiwa na mtoa habari lakini sio ninachokijua au kusikia kwa watu, nilimuuliza hii nyumba ni yako? akajibu kweli yeye ndio mmiliki sasa siwezi kubisha, magazeti yanakosea kusema mimi naipotosha jamii ya watanzania… sijaipotosha na kama kweli ile sio nyumba yake mimi sitakiwi kulaumiwa,” alikiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds Fm.
    “Kwenye show ya Take One ndani ya wiki mbili zijazo Wema amekubali kwamba atautoa uthibitisho kuonyesha kwamba ni mmiliki halali wa hiyo nyumba japo siwezi kuutaja ni uthibitisho gani,” aliongeza.

    No comments:

    3500K