• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, June 21, 2012

    TV za Kimataifa Zapagawa na Yideo ya AY



    Siku chache baada ya kuachia video yake mpya ya ‘Party Zone’ msanii wa kimataifa wa nchini Tanzania, Ambwene Yesaya aka AY, vituo vikubwa vya runinga duniania vimeanza kuipiga video hiyo kwa fujo huku ikiipigia promo pia kwenye mitandao ya kijamii.
    “Coming up on Crispy Fresh: Chris Brown, Coldplay ft Rihanna, Kanye West, AY ft Marcochali ‘Party Zone’,Neyo, Usher & 2freshLes,” iliandikwa jana kwenye ukurasa rasmi wa Twitter wa kituo cha Channel O cha Afrika kusini.
    Kipindi hicho cha ‘Crispy Fresh’ hupiga video mpya zilizoifikia TV hiyo na katika lisi ya nyimbo hizi za jana kama zilivyotajwa kwenyr orodha hiyo ni AY tu ndiye msanii kutoka Afrika ambaye wimbo wake upo katika awamu ya kipindi hicho na video zingine ni za wasanii wa Marekani.
    Baada ya kuitambulisha video hiyo ambayo AY kamshirikisha Marco Chali, kituo hicho jana kiliandika tena, “Catch @AY ft Marcochali ‘Party Zone’ again at 17:43pm & 20:04pm on Channel O today, Original African‬.”
    Wakati Channel O ikiendelea na promo hiyo ya video ya AY, kituo maarufu duniani kwa burudani cha nchini Ufaransa,TRACE nacho kiliipa shavu video hiyo, “Comin up this hour— the brand new @Ay ft Marcochali – Party Zone! Stay tuned…”
    Awali kabla ya jana TRACE Urban in Africa, iliitambulisha video hiyo kwa kuandika, “Stay tuned — coming up our EXCLUSIVE video – Ay ft marcochali “Party Zone” video! Only on TRACE Urban!”
    Kwa promo hiyo ambayo ndo kwanza imeanza ni sahihi mtangazaji wa Clouds Fm Reuben Ndege kumuuliza hivi AY, “money still has a crush on you au tayari umeibebesha money mimba ya mapacha pair 4??? Na yeye kujibu. “Hahaha nishapiga mimba so big movement r gwan.”

    No comments:

    3500K