Khamisi Tanga (46), ameota matiti katika hali isiyo ya kawaida
ikidaiwa imesababishwa na kutumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi
ARV’S.
Akizungumza na waandishi wa habari waliokwenda Wilayani humo
kufanya utafiti kuhusu utekelezaji wa sheria ya Ukimwi na Chama cha
Waandishi wa habari za Ukimwi (AJAT),Khamisi (Pichani) alisema alipatwa
na mkasa huo miaka mitatu iliyopita.
Akisimulia namna alivyoanza kuugua alisema awali aliona matiti
yake yakiongezeka ukubwa kila kukicha lakini hakujua kama lingeweza kuja
kuwa tatizo kubwa kama lilivyo sasa.
Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya ilimbidi kwenda kliniki
anayohudhuriaga kupata dawa na kuwaeleza manesi ambapo walimjibu kuwa
imesababishwa na dawa anazotumia na hivyo kulazimika kukatizwa dozi hiyo
na kupewa aina nyingine.
Hata hivyo Khamisi alisema kwamba pamoja na kubadilishiwa dozi
hajaona kama kuna mabadiliko yoyote aliyoyapata na kuongeza kwamba hivi
karibuni alipewa dawa nyingine ambazo kati ya hizo kuna zile ambazo
zilimsabishia matiti na tayari ameanza kupatwa na maumivu aliyokuwa
akisikiaga awali wakati matiti yalivyokuwa yanaanza kuota.
Kwa mujibu wa Khamisi ameshahangaika kupata matibabu hadi
Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili lakini hadi leo hajapatiwa tiba stahili
ya kumaliza tatizo hilo.
“Jamani Watanzania naomba wanisaidie kwa njia yoyote ile ili
niondekane na hali hii kwani inanidhoofisha sana na kunikosesha raha
hasa mbele ya wanaume wenzangu."Kwani hapa navyoongea na nyie waandishi nilipimwa hadi kansa na matiti ndio kama hivyo mnavyoyaona yanaendelea kukua na huniuma sana
hasa wakati ninapolala,”alisema kaka huyo.Pia alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya Kikwete kumsaidia ili
arudi katika hali yake ya uanaume kwa kuwa maisha kwa sasa kwake
yamezidi kuwa magumu kwa kuwa hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na
hali hiyo.
Mtaalam wa magonjwa, Dk. Dina Komakoma,akielezea kuhusu sababu za
kutokewa kwa hali hiyo kwa wagonjwa wenye maambukizi ya VVU ni jambo la
kawaida japo hutofautiana.
Dk. Komakoma alisema wengine hujikuta wakinenepa au wakikonda sana na
hili la Khamis sio mtu wa kwanza kupatwa na hali hiyo na kuongeza kwamba
inapotokea mgonjwa akapata hali tofauti kama hiyo anapaswa kusitishiwa
No comments:
Post a Comment