Nanukuu kutoka Take One ya Clouds Tv; “Marafiki ndio
wanaompoteza mwanangu Wema kwani ndio wanaomchimba na baadae kutoa siri zake
hadharani na magazeti yanapata kumwandika ili kupata pesa kupitia mgongo wa
mwanangu. Na sasa natoa muda wa mwezi mmoja tu kwa magazeti yote ya udaku
yatakapomwandika Wema wajue hawapambani na Wema bali wanapambana na mimi na
nitasimama nao kizimbani pamoja na mwanasheria wangu”. Huku akiendelea
kumzungumzia mwanae alisema kuwa marafiki ndio wanaomfanya mwanae awe na tabia
mbaya kwani wanamwendea kwa
waganga wanamfanyia madudu yao na kasha haohao ndio
wanaokuja kwake na kumwambia ampeleke Wema kwa mganga kusuruhisha matatizo
yake, Lakini mama Wema alitoa tahadhari kwamba sasa ameshamtengeneza mwanae
hivyo wake chonjo hawataweza kumfanya tena awe kama wanavyotaka wao na
kusisitiza kuwa hao marafiki wanaojidai kuwa ni kipenzi cha Wema ndio
wanaompoteza mwanae na yeye hapendi hata kuwaona kwani marafiki wa mwanae ni
familia yake tu!! Swali, Je rafiki aliyekura nae kiapo kwenye kipindi hikohiko
kilichoneshwa tarehe 19/4 je naye ana lengo la kumpoteza mwanae!?.
Wednesday, June 20, 2012
Home
Unlabelled
MAMA WEMA ATOA MWEZI NA ONYO KALI_TAKE ONE!
No comments:
Post a Comment