J
|
eshi la
Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuiba Ng’ombe
Jike mali ya JULIUS S/O MATHIAS mwenye
umri wa miaka 32, Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Michese.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma ZELOTHE STEPHEN alisema Tukio hilo
lilitokea mnamo tarehe 09/06/2012 majira ya saa kumi na moja (17:00 hrs)
jioni maeneo ya Kijiji cha Michese, Kata ya Mkonze Manispaa ya Dodoma.
Akizungumzia
tukio hilo
Kamanda Zelothe alisema toka Kuibwa kwa Ng,ombe huyo mlalamikaji hakuweza kutoa
taarifa kituo cha Polisi na badala yake aliendelea kumtafuta katika mazizi ya
wenzake hapo kijijini mpaka siku ya jumapili alipompata ndipo akatoa taarifa.
Kamanda
Zelothe alisema juhudi za kumtafuta Ng’ombe huyo zilifanyika kwa ushirikiano
wa pamoja wa mlalamikaji na wanakijiji wa eneo hilo bila kutoa taarifa
Polisi na walitafuta katika mazizi yote pale kijijini lakini
hawakufanikiwa.
Aidha
alisema siku ya Jumapili ya tarehe 17/02/2012 majira ya saa kumi na
mbili asubuhi alimuagiza mdogo wake aliyejulikana kwa jina la JOSEPH S/O
MATHIAS kuendelea kufuatilia, akiwa katika ufuatiliaji akakutana na
mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina la MOSES S/O MDOE mwenye umri wa miaka 20,
Mkulima, Mkazi wa Michese akiwa anamswaga Ng’ombe huyo kuelekea kijiji cha
Chiikwi.
Mkuu huyo
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
alisema hali hiyo ilipelekea wanakijiji hicho kukusanyika na kuanza
kujichukulia sheria mkononi kwa kuwashushia Kipigo watuhumiwa hao, lakini Raia
wema waliwahi kutoa taarifa Polisi ambao walifika mapema kuwaokoa na kipigo
kisha kuwakamata.
Kamanda
Zelothe Stephen alitoa wito kwa wananchi kuacha vitendo vya kujichukulia
sheria mkononi na badala yake kutumia dhana ya ukamataji salama na kutoa
taarifa mapema katika vituo vya Polisi ili hatua stahiki zichukuliwe.
Zelothe
alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa katika kituo cha Polisi kati katika
Manispaa ya Dodoma
na watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
No comments:
Post a Comment