K
|

Azam
ilianza mazoezi ya viungo na kusaka pumzi na stamina wiki mbili zilizopita,
Beach na Gym na wiki wanatarajiwa kuanza kuuchezea mpira.
Tayari
Azam, washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wamekwishamalisha
usajili wa wachezaji wao hata kabla ya kwenda likizo.
Programu ya maandalizi ya Kombe
la Kagame, inayoendelea hivi sasa itamalizika siku moja kabla ya kuanza
mashindano hayo, Juni 28 na yatakapomalizika, wachezaji watapewa mapumziko ya
siku chache kabla ya kuanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Maandalizi kwa ajili ya VPL
yatahusisha pia ziara ya nje ya nchi ya kujiandaa na msimu mpya, ingawa amesema
nchi hiyo itatajwa baadaye.
Wachezaji
wapya kikosini Azam msimu huu ni kiungo Mkenya George ‘Blackberry’ Odhiambo na
kipa Deogratius Munishi kutoka Mtibwa Sugar, wakati Aishi Salum, Jackson
Wandwi, Dizana, Ibrahim Rajab Jeba na Joseph Kimwaga, wamepandishwa kutoka
akademi ya Azam.

Viungo ni
Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, Abdi Kassim Sadalla,
Ramadhani Suleiman Chombo, Abdulghani Ghullam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz
Stima, Ibrahim Joel Mwaipopo, Kipre Tchetche, Mrisho Ngassa, Zahoro Pazi,
Khamis Mcha na George Odhiambo ‘Blackberry’ wakati washambuliaji ni Gaudence
Mwaikimba, John Bocco ‘Adebayor’.
No comments:
Post a Comment