Rais wa Mauritania amelitaja ombi la
wapinzani waliomtaka ajiuzulu uongozi kuwa ni ishara ya udhaifu wao.
Rais
Muhammad Ould Abdulaziz wa Mauritania amesema leo kuwa lengo la wapinzani
wanaomtaka aondoke madarakani ni kufunika kushindwa kwao kujipatia kura za wananchi.
Rais wa Mauritania ameongeza kuwa viongozi wa upinzani wote walishiriki kwenye
mchuano wa uchaguzi wa rais lakini walishindwa kupata kura za wananchi wa
Mautritania. Rais Muhammad Ould Abdulaziz amesema anataraji kuwashinda tena
wapinzani wake katika kila uchaguzi utakofanyika nchini humo. Rais Abdulaziz
amesisitiza pia kufungamana nchi yake na suala la kuwa na uhusiano mwema na
majirani zake na kueleza kuwa Mauritania haina tatizo lolote na majirani zake.
No comments:
Post a Comment