Edwin Rweyumamu kutoka
ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)
akimkaribisha CAG ambaye pia ni Mkaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa
(UN) Ludovick Utouh ili aweze kuongea na waandishi wa habari kuhusu
Tanzania kupata nafasi ya kukagua hesabu za UN kwa kipindi cha miaka sita.
Watumishi 60 kutoka ofisi ya CAG watafanya kazi ya kuzikagua taasisi 10 za
UN.
Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) ambaye pia ni Mkaguzi wa hesabu za Umoja wa
Mataifa (UN) Ludovick Utouh akiongea na waandishi wa habari kuhusu
Taasisi 10 za UN ambazo zitafanyiwa ukaguzi chini ya usimamizi wake ambapo
watumishi 60 kutoka ofisini yake watafanya kazi hiyo. Kwa kipindi cha miaka
sita nchi za Tanzania, China na Uingereza zimepewa jukumu la ukaguzi wa
hesabu za UN.
NA Anna Nkinda – HABARI MAELEZO
No comments:
Post a Comment