Gari ya kampuni ya Asas Iringa ikijaribu kutoa msaada wa kuvuta malori yaliyogongana ili kutoa maiti iliyobanwa na lori.
Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga akiwa katika eneo la tukio.
WATU
wanne wamekufa papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya malori
mawili kugongana na kutumbukia bondeni katika mteremko wa mlima kitonga
wilayani Kilolo katika barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam.
Maroli
hayo moja lenye shehena kubwa ya madini aina ya shaba na lingine lenye
bidhaa mbalimbali za dukani yanalindwa vikali na askari Polisi wa wilaya
hiyo, ili kunusuru mali hizo zisiibiwe.
Akizungumza
katika eneo la ajali Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Taifa,
Mohamed Mpinga alisema kwa masikitiko kwamba ajali nyingi zinazoendelea
kutokea nchini zimekuwa zikisababishwa na uzembe wa madereva.
Tarifa
kutoka kwa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio zimedai kwamba,
ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana na kuwa chanzo cha ajali hiyo
ni lori lenye namba za usajili T587 BGP aina la Scania.
Mashaka
Abdala alisema roli hilo lenye mali mbali mbali za dukani lilikuwa
limeharibika na kuegeshwa kando ya barabara hiyo na liligongwa na lori
lingine lenye namba za usajili T T319 BDG aina ya Scania pia ambalo
breki zake zilikataa wakati likitelemka katika mlima huo.
Akithibitisha
vifo vya watu waliokuwemo kwenye maroli hayo, Mpinga alisema taarifa za
Polisi zimethibitisha watu wanne kati ya sita waliokuwemo katika maroli
hayo kufa hapo huku mmoja akijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika
hospitali ya mkoa wa Iringa.
Mbali
na majina yao kutofahamika mara moja, mpaka tunakwenda mitamboni maiti
moja ilikuwa bado haijatolewa kutoka kwenye kibini ya moja ya maroli
hayo kilichopondwa na kufunikwa na kontena za maroli hayo, katika bonde
la mlima huo.
Taarifa
za kipolisi zimedai kwamba katika ajali hiyo kibini ya roli lilolokuwa
limepakia shaba lilifunikwa na kontena za maroli hayo baada ya kwa
pamoja maroli hayo kutumbukia katika korongo la mlima huo.
Ajali
hiyo ni moja kati ya ajali nyingi zinazoendelea kutokea mkoani Iringa
huku ukiwa katika maandalizi ya kitaifa ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani.
Kamanda
Mpinga aliwakumbusha madereva kuzingatia sheria za barabarani na
akahidi kwamba msako mkali wa wale wanaokiuka sheria hizo utaanza
kufanywa.
Mpinga
alisema kikosi cha usalama barabarani kitaweka utaratibu wa ukaguzi
maalumu wa magari katika maeneo ambayo ajali zimekuwa zikitokea mara kwa
mara ikiwa ni pamoja na katika mlima huo.
Chanzo: www.frankleonard.blogspot.com na http://francisgodwin.blogspot.com
Chanzo: www.frankleonard.blogspot.com na http://francisgodwin.blogspot.com
No comments:
Post a Comment