Aliyekuwa waziri wa
fedha nchini India Pranab Mukherjee ndiye rais mpya wa taifa hilo. Mukherjee
aliye na umri wa miaa 76 alipata ushindi huo baada ya kutangazwa kwa matokeo ya
uchaguzi wa urais uliofanyika wiki iliopita.
Rais
huyo mpya anayejulikana kama mchapa kazi, alijiunga na siasa za India
miaka ya 69.
Mwezi uliopita Mukherjee alijiuzulu kama waziri wa fedha wa
nchi hiyo baada ya kushikilia wadhifa huo kwa miaka mitatu. Alifanya hivyo ili
aweze kuwania kiti hicho cha Urais. Rais alichaguliwa na Wabunge wa majimbo na
taifa nchini India.
No comments:
Post a Comment