Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi
kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA)
uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Julai 21 mwaka huu).
Ushindi waliopata viongozi
waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
DOREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Dodoma.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano
wake kwa Kamati ya Utendaji ya DOREFA chini ya uenyekiti wa Nasoro Kipenzi
ambaye amechaguliwa kwa kipindi cha pili mfululizo.
Uongozi huo mpya una changamoto
nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani
Dodoma kwa kuzingatia katiba ya DOREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu
vilivyo juu yake.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya
Uchaguzi ya DOREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo
unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi waliochaguliwa katika
uchaguzi huo uliofanyika hoteli ya Dear Mama ni Nassoro Kipenzi (Mwenyekiti),
Thadeo Kaliza (Makamu Mwenyekiti), Stewart Masima (Katibu Mkuu), Kepha Maswaga
(Mhazini), Mulamu Ngh’ambi (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Mohamed Aden
(Mwakilishi wa Klabu TFF), Zawdi Kassim (Mjumbe Kamati ya Utendaji).
No comments:
Post a Comment