M
|
wanafunzi wa Shule ya
Msingi Mlimanjiwa na mkazi wa Kijiji cha Mlimanjiwa,Wilaya ya Chunya Mkoani
Mbeya Mussa Manyesa(9),amefariki dunia kwa kutumbukia katika shimo la maji katika
mgodi unaomilikiwa na Mrs Kasaka wa wilaya hiyo na kusimamiwa na Isaack
Msowoya.
Tukio hilo limetokea Juni 16 majira
ya saa 10 jioni,wakati mtoto huyo akiwa na wenzake na alipopita kando kando ya
shimo hilo
alitumbukia na kupoteza maisha papo hapo.
Baba wa mzazi wa marehemu Bwana Leonard Manyesa,amesema wakati wa
tukio hilo alikuwa nyumbani kwake na muda mfupi alipata taarifa za mwanae
kufariki,hali iliyompelekea kufika eneo la tukio,kisha kutoa taarifa kwa
Mwenyekiti wa kijiji Bwana Shaban Masa.
Polisi walifika eneo la tukio na kuthibitisha kifo hicho na
kuwaruhusu ndugu wa marehemu kuuchukua mwili wa marehemu na mazishi ya kuuaga
mwili huo yalifanyika Juni 17 mwaka huu kijijini hapo.
No comments:
Post a Comment