Kambi ya Ahmed Shafiq, Waziri Mkuu wa
mwisho katika utawala wa dikteta Hosni Mubarak nchini Misri imetangaza kuwa
Shafiq anaongoza kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliofanyika Jumamosi
na Jumapili.
Timu
ya kampeni ya Shafiq imesema mgombea wake anaongoza kwa wingi wa kura na hivyo
kupinga tangazo la hapo awali la harakati ya Ikhwanul Muslimin kwamba mgombea
wake Muhammad Morsi ndiye aliyeshinda kwa kupata asilimia 52 ya kura. Hata
hivyo, duru nyingi za habari zinaripoti kuwa Morsi ndiye anayeongoza. Matokeo
rasmi yatatangazwa siku ya Alhamisi. Huku hayo yakijiri, Baraza la Kijeshi
nchini Misri limetoa taarifa na kusema kuwa rais mpya atakuwa na madaraka ya
wastani ikilinganishwa na Hosni Mubarak. Jeshi limesema Rais hatokuwa Amiri
Jeshi Mkuu, rais pia hatoweza kuanisha bajeti ya nchi na kwamba mamlaka ya
bunge lililovunjwa na mahakama yataendelea kubakia mikononi mwa jeshi.
No comments:
Post a Comment