Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager leo imeibuka na ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya
wenyeji Chad katika mchezo uliomalizika jioni hii katika uwanja wa
Omnisport Idriss Mahamat Ouya uliopo jijini N’Djamena.
Kikosi cha Stars kilicheza vizuri kwa maelewano kwa lengo la kusaka bao la
mapema, safu ya ushambuliaji ilikuwa mwiba kwa walinzi wa Chad katika
dakika 30 za kipindi cha kwanza na kukosa nafasi zaidi ya nne za wazi
kupitia kwa Ulimwengu, Farid, Samatta na Kazimoto
No comments:
Post a Comment