Akipiga stori kwenye kipindi cha eNEWS kinachorushwa na ting'a namba moja
kwa vijana (EATV) Linah Sanga alisema kuwa toka kipindi cha nyuma alikuwa
anatamani kuwa na msanii huyo kama mpenzi wake, ingawa anadai mpaka sasa
ndoto yake hiyo haijaweza kukamilika mpaka dakika hii.
"Unajua nilikuwa namu admire Wizkid toka muda mrefu, na ndiyo mwanaume
ambaye hata ukiniuliza ni msanii gani wa kiume katika bara la Afrika ambaye
ungependa kuwa naye au ambaye nampenda nitakwambia ni Wizkid, siwezi
kukataa ila ndiyo hivyo tena maana mwenyewe natamani ingekuwa kweli"
alisema Linah Sanga
No comments:
Post a Comment