*Jana wakimbizi kutoka katika kambi za Nyarugusu na Nduta zilizopo mkoani
Kigoma waliungana na watu wengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya maji
duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni maji safi kwa maendeleo endelevu.*
*Maadhimisho hayo yaliandaliwa kwa ushirikiano kati ya serikali kupitia
idara ya wakimbizi na mashirika mbalimbali yanayotoa misaada katika makambi
hayo yakiwemo UNHCR, UNICEF, International Rescue Committee, Oxfam,
TWESA, Save the Children, Water Mission, TCRS na mengine mengi.
No comments:
Post a Comment