• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Sunday, December 1, 2013

    huyu ndiye mshindi wa EBSS 2013 Emmanuel Msuya jamaa hapo kati


    Shindano la Epiq Bongo Star Search 2013 linafikia ukingoni leo usiku (November 30), ambapo mmoja kati ya washiriki watano walioingia fainali atatangazwa kuwa mshindi.
    Kila mshiriki ana sifa za pekee ambazo zinamtofautisha na washiriki wengine na huenda ikamsaidia kuibuka mshindi.
    Jina moja kati ya majina haya litapamba vichwa vya habari kesho.
    Emmanuel Msuya:     
     Ni mshiriki namba 21 anaewakilisha kanda ya ziwa. Ndiye mshiriki pekee wa kiume ambaye ameingia fainali akiwa na uwezo mkubwa wa kuimba, lakini kitu kikubwa kinachomtofautisha na wenzake ni uwezo mkubwa alionao wa kupiga vyombo vya muziki kama kinanda na gitaa.
    Msuya amerekodi wimbo unaoitwa ‘Leo Leo’ ambao ameufanya na Producer Sheddy Clever.
    Elizabeth Mwakijambile:
    Sifa moja kubwa aliyonayo inayomtofautisha na wenzake ni uwezo wake mkubwa wa kubadili sauti nakuimba vizuri sauti ya base (ya kiume), mbali na vocal ya nguvu ya kike aliyonayo.

    Mara kwa mara anapoimba unaweza kuifananisha sauti yake na ya mwanamuziki mkongwe Stara Thomas.
    Elizabeth amerekodi wimbo unaoitwa ‘Nifanyeje’ uliotayarishwa na producer Lamar wa Fish Crab.
    Maina Thadei:
    Uwezo mkubwa alionao wa kuimba nyimbo za taarab na miduara umemfanya kuwa na ladha tofauti na wenzake na kujikombea fans wengi wanaopenda aiana hiyo ya muziki.
    Sio tu aina ya muziki anaochagua, lakini performance yake awapo jukwaani na mbwembwe za aina yake ni kitu ambacho kitakufanya umuangalie hadi anaposhuka jukwaani.
    Maina amefanya wimbo wa mduara unaitwa ‘Panya Buku’, na ukisikiliza utahisi unasikiliza wimbo wa msanii mzoefu kwenye miondoko hiyo.




    Melisa John:
    Aliingia kwenye mashindano haya kwa njia tofauti, kwa kupiga simu na kukubalika kuungana moja kwa moja na washiriki wengine ambao walikuwa wameshapitia mtindo wa kupanga foleni na kuimba mbele ya majaji.
    Hakika sauti yake iliyowavuta majaji kwa njia ya simu imeendelea kukimbiza na hasa anapoimba nyimbo za waimbaji wakubwa kama Alicia Keys. Sauti yake imemgusa moja kati ya viongozi wa studio kubwa (jina tunalo) ambaye aligusia swala la kutaka kufanya nae kazi. Huenda akapata deal hilo baada ya shindano hilo.
    Melisa mefanya wimbo unaoitwa ‘Ah Ah’ na producer Lamar. Ni wimbo flani wa ‘mbele hivi kiaina’ wanasema watoto wa mjini. Na amejaribu kurap pia.
    Amina Chibaba:
    “Mimi ni mshiriki pekee ambaye nimepitia changamoto nyingi sana, yaani nyingi mno. Kule kukataliwa na majaji, Salama alivyokuwa ananiambia ‘Ukubwa wa Boflo’, Master Jay ‘simfikishi’ ni challenge ambazo zimenifikisha hapa nilipo.” Amina Chibaba aliiambia Tovuti ya Times Fm.
    Lakini mbali na changamoto zote alizopia mshiriki huyu namba 03 anajiamini na anaamini uwezo wake.
    “Lakini naamini nina kipaji, naweza na nimshiriki pekee ambaye naweza nikakulaza kama umekaa na nikubembeleza kwa sauti yangu.”
    Je, nani atatangazwa kuwa mshindi wa EBSS 2013 leo? Swali hili litapatiwa majibu pale Escape 1, Dar es Salaam kabla hakujapambazuka.

    No comments:

    3500K