Baada
ya fans wengi kuanza “kumponda” mwanadada Irene Uwoya kuwa gari aina ya
Range Rover aliyoinunua “amehongwa na washika dau”, mwanadada
huyo ameibuka na kusema kuwa mali anazomiliki amezinunua kwa pesa
zake anazopata kwenye uigizaji pamoja na zile zinazotokana na biashara zake nyingine.
zake anazopata kwenye uigizaji pamoja na zile zinazotokana na biashara zake nyingine.
“Kwa
nini watu hawataki kukubali kuwa kazi ya uigizaji inalipa, yaani sisi
tukinunua magari tumehongwa? Yaani wa kuhongwa ni sisi tu na si tasnia
nyingine?” alihoji Uwoya. Aidha
Uwoya alisema kuwa kazi ya filamu ukijua kuitumia vizuri kwa kujiwekea
malengo na kuitumia vizuri kila senti unayoipata, unaweza kupata
mafanikio makubwa.“Tunaigiza
sehemu nyingine ambazo hutaki hata mwanao aone, hii siyo kazi rahisi
maana yake ni kwamba kama ukiipatia unaweza kujikuta unaingiza pesa kila
siku kwani mwaka mzima uko kazini,” alisema Irene amesema kuwa ameamua kuweka wazi ukweli huo kutokana na maneno yaliyozagaa kuwa magari anayomiliki amenunuliwa na wanaume
No comments:
Post a Comment