"Kikubwa niliona ni mtu ambaye ana moto, unajua mtu anapokuwa ameanza halafu ana moto obvious anataka kufanya vitu vizuri vikubwa yaani damu inachemka unaweza kusema anatafuta exposure pia," amesema Ben Pol
"Kwahiyo nilimpa kwa sababu hizo, kwa sababu niliona yeye kazi zake za mwanzo alizozifanya za akina MABESTE za akina nani ni kazi kali sana. Anafanya kwa nguvu sana na ubora wa hali ya juu.
Kwahiyo nikaona huyu mtu akipata audio nzuri anaweza kufanya kitu kikubwa ndio maana nikafikiria kumpa. Nikaona bado ni mpya, bado ana njaa, bado ana ubunifu mwingi, unajua tofauti na ukimpa director ambaye ameridhika ana miaka mitano, kumi katika industry anaweza akakufanyia kama moja ya kazi zake za kila siku kwa hiyo mimi nilikuwa naiepuka. Kwahiyo mimi nilikuwa nataka kama mtu unampa kazi afanye kazi hiyo hiyo pekee yake."
No comments:
Post a Comment