• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Friday, December 14, 2012

    Aibu-Baby Madaha Ashindwa kulipa Kodi ya Nyumba




    KIPINDI hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka watu wamekuwa wakisumbuliwa na ishu kibao ikiwemo ya kodi za nyumba, ambapo hadha hiyo imemkumba msanii wa filamu na muziki Baby Madaha ambaye amepewa notes ya siku mbili awe amelipa kodi anayodaiwa ikiwa ni sh milioni mbili, za kipindi cha miaka mitatu.

    Taarifa za uhakika zilizofika kwa mwandishi wetu  zinasema kuwa msanii huyo hajalipa kodi zaidi ya miaka ya mitatu, huku mwenye nyumba akiwa anampa ahadi hewa kuwa atalipa kesho bila mafanikio yoyote kitu ambacho kimemlazimu mwenye nyumba kutoa makucha yake na kumpa siku hizo mbili awe amekamilusha deni hilo.

    Hata hivyo taarifa hizo zinadai kuwa msanii huyo hajaonekana nyumbani hapo maeneo ya Kinondoni kwa siku tatu, lakini kutolewa kwa notes hiyo alijulishwa kwa njia ya simu.

    Mtoaji wa ishu hiyo ambaye anaishi mazingira ya tukio hilo alisema kuwa baba mwenye nyumba awali kabisa alitaka kutoa vitu vya msanii huyo nje lakini kutokana na uvumilivu wake aliacha na aliamua kumpigia simu kuwa anampa siku mbili awe amelipa kiasi hicho cha pesa bila hivyo aondoe vitu vyake.

    “Inatia aibu sana kwa msanii mkubwa kama huyo kudaiwa pesa ndogo kiasi hicho, mwenye nyumba awali kabisa alitaka kutoa vitu vyake nje lakini kutokana na hekima yake aliacha na alimpigia simu kuwa anampa siku mbili awe amelipa kiasi hicho cha pesa bila hivyo anamfikisha mahala husika,” kilisema chanzo hicho.

    Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alimtafuta Baby Madaha ili kueleza juu ya taarifa hizo, ambapo alidai kuwa amepokea simu hiyo kutoka kwa mwenye nyumba ikimtaka kulipa kiasi hicho cha pesa, lakini juu ya kutolala ndani ni ishu ya uongo.

    Alidai kuwa hajashindwa kulipa hela hizo lakini alikuwa na mipango yake anaifanya kwani hawezi kudhalilishwa kwa pesa ndogo kiasi hicho hata kama anaishi kwenye nyumba ya kupanga.

    No comments:

    3500K