"Tarehe 10 ya mwezi wa 11 siku ya juma mosi ni moja ya siku ambazo sitozisahau maishani mwangu.
Baada
ya kumaliza majukumu yangu ya kila siku, nilikwenda masaki kumwona
mmoja wa jamaa zangu wa karibu nikiwa na Blogger wangu Bestizzo pamoja
na mwanafamilkia ya wasafi Dumi(Dancer) Mishale
ya saa moja hivi nikiwa maeneo ya masaki karibu na kona ya msasani
nilipata ajali ambayo haikuwa kubwa sana ingawa imesababisha uharibifu
kwa kiasi kikubwa, Kama mjuavyo barabara ya msasani ni ndogo na gari
huwa haziko katika mwendo wa kasi... ghafla dereva wa pikipiki
alikatisha mbele yangu na katika kujaribu kumkwepa nikagonga gari ndogo
aina ya Rav 4 ambapo ilisababisha dereva wa pikipiki kuanguka katikati
ya gari zote mbili. Hiyo ndio hali halisi ya ajali niliyokutana nayo
jumamosi iliyopita"
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutunusuru wote bila majeraha makubwa zaidi ya maumivu tu ya hapa na pale.
No comments:
Post a Comment