Kiongozi
wa zamani wa taifa la Cambodia Mwana mfalme Norodom Sihanouk
amefariki mjini akiwa na umri wa miaka 89.
Naibu waziri
mkuu wa Cambodia Nhek Bun Chhay amesema
kuwa Sihanouk amefariki kutokana na uginjwa
wa moyo. Sihanouk aliongoza kampeni kwa
nchi yake kupata uhuru mwaka 1953
kutoka Ufaransa , na alichaguliwa kuwa mkuu
wa nchi mwaka 1960. Miaka kumi baadaye
aliangushwa kutoka madarakani katika mapinduzi yaliyoungwa
mkono na Marekani. Akiwa uhamishoni nchini
China alijihusisha na kundi la Khmer
Rouge, na baadaye alihitilafiana na utawala
huo wa kikomunist wenye msimamo mkali, na
kuishi kwa miaka 12 zaidi nchini China. Alijivua
madaraka yake ya ufalme mwaka 2004 kutokana
na afya yake kuwa mbaya. Hivi sasa Mtoto wake
mkubwa , Norodom Sihamoni, ndie mfalme wa Cambodia.
No comments:
Post a Comment