Mwili wa aliyekuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (52), utaagwa leo, Oktoba
15, 2012, katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Taarifa
iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa jeshi hilo mkoani humo Lilian Matola,
imesema kwamba shughuli ya kuaga mwili huo itaongozwa na Mkuu wa Jeshi la
Polisi Nchini, Inpsekta Jenerali Saidi Mwema.
Matola
alisema leo kwamba, viongozi wengine wa kiserikali watakaoshiriki ni pamoja na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, William Lukuvi,
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, wakuu wa wilaya na viongozi
waandamizi wa jeshi hilo.
Alisema
kuwa shughuli za kuaga zitaanza saa 3:00 asubuhi baada ya mwili kutolewa katika
Hospitali ya Rufaa ya Bugando na kupelekwa kwanza nyumbani kwake Pasiansi.
Baadaye
saa 4:00 hadi saa 6:00 mchana itafanyika Ibada ya kumuombea kabla ya kusomwa
kwa wasifu wake na salamu kutoka kwa IGP, Makamanda wa mikoa mingine na
viongozi mbalimbali vya Vyama vya siasa.
Matola
alisema kuwa, mwili wa marehemu Barlow utasafirishwa mchana kwenda jijini Dar
es Salaam ambako taraibu nyingine za kuomboleza zitafuata kabla ya kusafirishwa
kwenda mkoani Kilimanjaro kwa taratibu za maziko.
No comments:
Post a Comment