• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Monday, September 3, 2012

    Uchambuzi wa Kina wa Wimbo mpya wa Ben Pol-Pete





    Wiki mbili zilizopita, Ben Pol ameachia ngoma mpya iitwayo Pete. Ni ngoma ya kwanza tangu ajiondoe MLAB. Panel ya TMP inauchambua kama ifuatavyo wimbo huu.


    Nani hajasubiri kwa hamu ujio wa Ben Pol nje ya Mlab?????!!!

    Hili ni toleo la kwanza kwake nje ya MLAB, naamini wengi mmelijua hili sasa ama baada ya wimbo huu kutoka, haya mmeshajua sasa twende pamoja!

    PETE- Title nzuri ambayo inautambulisha wimbo kuwa ni wa mapenzi ya kwa walio ndani ya ndoa (kwahiyo tulio ndani ya ndoa tumeupokea wimbo tofauti na nyie ambao bado mpo mpo) nawatania tu!!!

    Pongezi kwa watunzi wa wimbo huu kwa maneno mepesi ya kueleweka na zaidi kwa mtunzi wa sauti kwa kuja na melodies nzuri na nyepesi kushikika.

    Huwa sina shida na Ben katika uimbaji….ni kijana anayeijua kazi yake haswaaa na ana hisia zoooote zinazohitajika katika wimbo.

    Hapa changamoto kubwa ipo katika production…siku zote nasema sina maneno ya kitaalamu kufafanua matatizo lakini nina sikio langu ambalo mara nyingi halinidanganyi…punde nimeshuka kwenye gari nikiwa nimeshasikiliza nyimbo zote za Ben nizipendazo, playlist ilikuwa hivi 1. Nikikupata 2. Maumivu 3. No.1 Fan. 4. Samboira 5. Maneno 6. Maboma (my favourite) 7. PETE….haya ngoja niseme sikio langu lilivyojibu baada ya “mlinganisho” wa sita za Mlab na hii ya Mona Gangster. Kiukweli kabisa mpishano upo, si katika uimbaji wa Ben bali katika usikikaji wa muimbaji na vyombo vilivyopigwa katika mdundo

    Tusisifiane visivyo kwakuwa hatutafikishana popote kimaendeleo, Ben katika Pete hasound vizuri kama Ben katika Maboma….chukua hii kama changamoto na fanya kuongeza umakini wakati unaamua wapi urecord ama ngoma gani uachie tusikie.

    Leo niingie kwenye utunzi kidogo, nimeacha kooote nimeenda mwishomwisho mwa wimbo huu unapopatikana mstari ufuatao:-

    “Pete kidoleni mwako yanisuta mweziooo”

    Napata shida kidogo kwamba kwanini pete aliyovaa mtu mwingine imsute yeye ikiwa kusutwa ni kitu cha ndani zaidi ambacho mtu atajisikia kutokana na hali halisi inayokinzana na matarajio….kwahiyo “msuto” ungekuwa ni wale watu waliosema mwanzo kwamba wasingedumu then ingekuwa sahihi lakini kama nia ni kuonyesha namna unavyojisikia ukiiona kidoleni mwake basi neno/hali sahihi pale AIBU.

    Kwahiyo ingekuwa ni mimi kwenye line hii ningesema “pete kidoleni mwako, yaniaibisha mwezio”

    Kwenye mstari unaofuatia “kwamaana nikukosapo Moyo wanienda mbio”…mstari huu unaonyesha kuwa na uhusiano na mstari uliopita (“Pete kidoleni mwako yanisuta mweziooo”)…na kinacholeta mahusiano hayo ni neno “kwamaana”…sasa hapa shida yangu ni kutoendana kwa mistari hii yenye uhusiano na hivyo kusababisha ubatili wa uhusiano wao. Kwa kufafanua ili ieleweke vizuri ni kwamba kinachomaanishwa hapa ni kuwa kinachofanya pete imsute ni vile moyo unavyoenda mbio pindi amkosapo.

    Watunzi wengi wamekuwa na tatizo hili, wakati mwingine hutokea pasi kutambua lakini mara nyingi tatizo hili hutokea wakati mtunzi anajaribu kutengeneza vina…kwa kusema hivi nishauri watu wakati wafanyapo tungo zao basi wasisahau kubakisha maana pindi wahangaikapo kutafuta vina…ni heri vina vikosekane ili maana ibaki kwakuwa kwenye wimbo maana ndiyo inamashiko.

    Tutoke huko kwenye tungo…

    MWISHONI  BEN ANAONGEA KUSEMA “new ben pol”
    niseme kitu kimoja kwamba uimbaji na mistari ni vitu vinavyoweza kumtambulisha muimbaji kitabia kwa hadhira yake (japo si sana). Tazama mistari na uimbaji wa Dully…mtazame Ney wa Mitego, mtazame Ferooz wa kipindi kile n.k. Kwa observation yangu ninadiriki kusema kwamba BEN POL amepokelewa kama kijana mmoja mpole, mnynyekevu, mwenye upendo na asiye na makuu…hii ni kutokana na jinsi alivyotengenezwa kuanzia mwanzo wa carrier yake.

    Kwa waliobahatika kuisikia album iliyopita ya Ben “MABOMA” watakuwa mashahidi kwamba hawajasikia sauti ya Ben ikitamka neno lingine ambalo halipo kwenye wimbo mf kujifagilia au hata kumtaja producer(KASORO MMOJA TU “higher” AMBAO KIUKWELI SI WA IDENTITY YA BEN

    Binafsi nilipenda sana maamuzi ya kutoongeaongea kwenye nyimbo kwani naamini kizuri hujiuza na pia hata wengi wenye heshima kimataifa huwa hawana mambo hayo.

    USHAURI WA BURE KWAKO BEN usilete upya wa kuongeaongea kwenye nyimbo, leo umeanza maneno mawili kesho matatu kisha utanogewa kabisa…nakusihi acha, acha kabisa, achaaaaa!!

    Na mwisho nimalize kwa kusema wimbo huu ni mzuri na kwa kiasi kikubwa unaonyesha njia ni nzuri kwa Ben kupita katika eneo hili la ALBUM YA PILI…felicitations.

     JRider
    Vocals zimekaa safi, ndio kitu cha kwanza nilichokisikiliza.

    Kuanzia mwanzo unaweza skia sound ya scratch..ambayo pia inaendelea hadi mwisho verse ya kwanza, also kwenye verse zingine, na hiyo scratch ina more lower frequencies ambazo ilibidi ipunguzwe na EQ.

    On top of that waliongeza Reverb kidogo na Delay, na kwenye most Effects kama hizi Reverb na Delay kuna Low Pass Filter na High Pass Filter kwa lugha rahisi nitaita EQ, na kwa kutumia hizi he was supposed to reduce and cut the Lower Frequencies on the Low Pass Filter ya Reverb ama Delay.

    Inasaidia kwamba hiyo sound ikiwa ina delay mfano.. basi feedback yake inakua tu za High Frequencies. Hii iko deep sana na sio rahisi wengi kujua. So give it a try and listen how the Low and High freqs sound on the Reverb Return when tweeked around...

    Nyimbo kwa ujumla iko safii, sina tatizo nayo sana.

    Pia kwenye izo Rhodes ingeongezwa Tremolo effects naona ita sound poa zaidi.

    Kuna guitar ambayo ipo recorded live, katikati...wangeongeza volume yake kidogo, 'cuz sio rahisi kwa listener kujua hata kama ipo.

    Ben Pol this time round ameamua kwenda na sound tofauti na tulivyomzoea previously, kwa jinsi nilivyosoma ni kwamba his next album atafanya na Music Producers wengine.

    Na kwa upande wa producer wa hii ngoma, ...kafanya freshiii... Big ups.

    SOURCE

    No comments:

    3500K