Hali hiyo imekuja baada ya kampuni hiyo kuvamia eneo la wakazi wa Ilomba Machinjioni na kuanza kuchimba vifusi kwa ajili ya kujengea barabara katika kiwanja ambacho kina mgogoro wa muda mrefu. Kenneth Mwang’amba ambaye ndiye anayedai kulimiliki eneo la kiwanja hicho chenye hati miliki yenye namba 2459 alisema kitendo walichofanya wachina hao kufanya shughuli za uchimbaji katika eneo lenye mgogoro ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Mwang’amba amesema eneo hilo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu kati yake na Skauti Mkoa wa Mbeya ambao walivamia eneo hilo bila kufuata taratibu ambapo mamlaka zinazohusika zimeshindwa kutoa ufafanuzi kuhusu nani ndiye mmiliki halali wa eneo hilo. Amesema baada ya kukosa maelewano kati ya Skauti na yeye Mwang’amba, Halmashauri ya Jiji iliamua eneo hilo lichukuliwe na Skauti ambapo pia walitakiwa kulipa fidia kwake baada ya makubaliano kutokana na uharibifu uliokuwa umetokana. Ameongeza kuwa kutokana na Skauti kushindwa kulipa fidia hivyo hawakuwa na uhalali wowote wa kuendesha shughuli ya aina yoyote katika eneo hilo kutokana na Skauti kushindwa kulipa fedha walizokuwa wakidaiwa. Kwa upande wake Msemaji wa Skauti Mkoa wa Mbeya Uswege Kagubo Mwaitebele ambaye pia ni mkufunzi wa Skauti alisema waliwaruhusu wachina kuchimba eneo hilo kwa makubaliano ya kuwajengea kituo cha kufundishia skauti hivyo hawakuona sababu za kusubiri. Kuhusu mgogoro uliopo kati ya Skauti na Mwang’amba, Mwaitebele alikiri kuwepo kwa mgogoro huo ambapo naye alisema eneo hilo linamilikiwa kihalali ingawa walishindwa kulipia fidia kama walivyokubaliana. Naye Afisa ardhi wa Jiji la Mbeya Ephraimu Mkumbo amekiri kuwepo kwa mgogoro wa eneo hilo huku akiwatupia lawama Skauti kwa kufanya shughuli zao kinyume na taratibu ambapo alisema wameshindwa kuonesha hata ofisi zao zilipo kwa ajili ya ufuatiliaji wa madai hayo.
Mkumbo alisema Halmashauri ya Jiji iliwaamuru Skauti kulipa fidia za eneo hilo kwa mhusika kama watahitaji kulimiliki kihalali ambapo alisema wamekuwa wakipiga chenga bila taarifa zozote hadi leo unapoibuka mgogoro mwingine. Kuhusu kuruhusu machimbo katika eneo hilo Mkumbo alisema Wachina ndiyo wenye makosa kwani walishapangiwa eneo la kuchimba vifusi ambalo lipo Kawaetere nje kidogo ya Jiji la Mbeya ambapo amesema kwa kufanya hivyo wamekiuka sheria na wanbachofanya ni uharibifu wa Mazingira.
No comments:
Post a Comment