AFRICA FOOTBALL NEWS: ETO'O AGOMA KUJIUNGA NA TIMU YA TAIFA CAMEROON
Samuel
Eto'o amekataa kuichezea Cameroon katika kutekeleza mgomo wake dhidi ya
kile alichokiita "mpangilio mbovu na mazingira yasioeleweka" katika
kikosi cha timu ya taifa.
Mshambuliaji huyo alikuwa kwenye kikosi cha
Cameroon kwa ajili ya kupambana na Carpe Verde katika michuano ya kufuzu kombe
la mataifa ya Afrika mwezi September baada ya kumaliza adhabu yake kufungiwa
miezi nane. Lakini Eto'o alisema kwenye barua yake aliyoiandikia shirikisho la
soka la Cameroon hatoweza kurejea kwenye timu ya taifa kwa sababu matatizo yote
yaliyomfanya akafungiwa bado hajatafutiwa ufumbuzi. Eto'o, ambaye ameshaichezea
nchi yake mechi 109 na kufunga mabao 54, alifungiwa kutokana na kuongoza mgomo
wa wachezaji baada ya kutolipwa posho zao. Shirikisho la soka la Cameroon
liliamuarifu Eto'o na mwanasheria wake pamoja na timu yake ya Anzhi Makhachkala
kwamba kifungo chake kimeisha mapema wiki hii. Wakati huo huo kocha Denis
Lavagne akamchagua Eto'o katika kikosi chake cha wachezaji 23 kwa ajili
ya kucheza dhidi ya Cape Verde tarehe 8 mwezi ujao kwenye mchezo wa raundi ya
kwanza ya kufuzu kushiriki AFCON 2013. Lakini nahodha wa Cameroon bado amekosa
furaha dhidi ya masuala ya uongozi mbovu kwenye timu ya taifa na suala lao la
kuwapandisha wachezaji ndege daraja la pili tena kwenye safari ndefu - na
kutokana na sababu hizo mshambuliaji huyo wa zamani wa Barca amejiondoa kwenye
timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment