Mwanamke
mmoja wa nchini Afrika Kusini ametiwa mbaroni baada ya kuwasumbua majirani kwa
muda mrefu akifanya mapenzi na mbwa wawili na pia akirekodi video akifanya
mapenzi na mbwa hao.
Mwanamke mmoja mkazi wa
Pretoria nchini Afrika Kusini amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za ukatili kwa
wanyama baada ya kugundulika kuwa kwa muda mrefu amekuwa akifanya mapenzi na
mbwa wake wawili. Mwanamke huyo mzungu mwenye nywele za hudhurungi alitiwa
mbaroni siku ya jumatatu baada ya malalamiko ya mwanamke huyo kufanya mapenzi
na mbwa kupelekwa kwenye taasisi ya kulinda wanyama. Kwa mujibu wa vyanzo vya
polisi, mtu mmoja ambaye hakutaka kugundulika alipeleka DVD ya mwanamke huyo
akifanya mapenzi na mbwa kwenye taasisi ya kutetea haki za wanyama ambayo
iliamua kupeleka suala hilo polisi. Polisi walipewa kibali cha kuisachi nyumba
ya mwanamke huyo ambapo DVD nyingi sana za mwanamke huyo akifanya mapenzi na
mbwa zilipatikana. "Inavyoonekana alikuwa akirekodi video za mapenzi yake
na mbwa kwa muda mrefu sana. Alitiwa mbaroni muda mfupi baada ya nyumba yake
kusachiwa", kilisema chanzo cha polisi. Mwanamke huyo alipandishwa
kizimbani siku ya alhamisi ambapo hakimu aliamuru mwanamke huyo apimwe akili
zake kabla ya kesi hiyo haijaendelea zaidi. Akitoka mahakamani baada ya
kulipiwa dhamana na rafiki yake wa kiume, mwanamke huyo alijificha sura yake
kwa kutumia gazeti ili waandishi wa habari wasimpige picha.Mbwa waliokuwa
wakifanya mapenzi na mwanamke huyo wamechukuliwa na kupelekwa sehemu nyingine
kwa uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment