Habari
kutoka miji ya Nairobi na Mombasa nchini Kenya zinasema kuwa, Waislamu
wanapanga maandamano makubwa katika miji hiyo punde baada ya Sala ya
Ijumaa hii leo kulalamikia mauaji ya viongozi na wanaharakati wa Kiislamu.
Duru
za polisi jijini Nairobi zinasema kwamba, maafisa wa kuzima fujo
wamewekwa katika hali ya tahadhari iwapo maandamano hayo yatageuka na
kuwa fujo. Mkuu wa polisi jijini Nairobi amesema hakuna kibali
kilichotolewa kwa ajili ya maandamano hayo lakini Waislamu wamesisitiza
kuwa wataandamana. Mwanaharakati wa Kiislamu, Sheikh Aboud Rogo aliuawa
siku ya Jumatatu mjini Mombasa na watu wasiojulikana. Mauaji hayo
yalizusha machafuko na fujo baada ya vijana wenye hasira kuandamana na
kuchoma moto makanisa mjini humo. Maafisa wanne wa polisi tayari
wameuawa kwenye fujo hizo za Mombasa
Friday, August 31, 2012
Home
Unlabelled
AFRICA POLITICAL NEWS: WAISLAMU MOMBASA KUANDAMANA LEO BAADA YA SALA YA IJUMAA
No comments:
Post a Comment