• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, July 4, 2012

    MFAHAMU ANAYEWAPA KIBURI NA CHANZO CHA JINA P SQUARE.


    Najua wengi mnaliona jina Jude Okoye kwenye video nyingi za P Square lakini msijue huyu ni nani na anatokea wapi, Kwa jina kama nilivyomtaja hapo ni mwanamuziki,prodyuza na director ambaye asili yake ni kule nchini Nigeria. Mwaka 1994 alianza kuvutiwa na kazi za filamu hivyo alianza kudirect filamu nchini humo ambapoa alifanya kazi kadhaa za filamu nchini humo lakini mnamo mwaka 1996 Jude alijikita kwenye sanaa ya music na alianza kufanya kazi zake mwenywe na alifanya kazi kama remix ya Chakademus na Pliers ambapo alikuwa akipewa msaada mkubwa wa kifedha na rafiki yake Hillary Ezeadilije. Miaka saba baadae alihamia Lagos ambapo ndipo alipojuana na P square wakiwa chuoni na mara ya kwanza kujua vipaji vya wawili
    hawa ni kwenye concert za chuoni hapo baaada ya kuwaona wakipafomu nyimbo ya Michael Jackson Smooth Criminal na nyimbo nyingine za msanii huyo na ndipo alipoanza kuwashauri waanza kufanya nyimbo zao wenyewe ila hawakuwa na jina kamili la kuliita kundi lao. Lakini wakiwa wanapafomu nyimbo yao ya kwanza inayoitwa They don kolo kwenye Club moja ya usiku huko MC wa siku hiyo hakupenda kuyataja majina yao yote wawili kila muda hivyo kwa vile wote majina yao yanaanza na P akatumia P square akimaanisha P'ETERE na P'aul na ndipo jina hilo lilipoanza kutumika rasmi mnamo mwanzoni mwa miaka ya 2000 na hapo ndipo alipoanza kazi za kutengeneza nyimbo na video za wasanii hao hadi hii leo amewafikisha hapo walipo.

    No comments:

    3500K