Taifa la Burundi limemtunukia Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere Tuzo la juu kabisa ambayo Burundi hutoa kwa watu
mbali mbali kutokana na mchango wao katika kuleta uhuru na baadaye kwa jitihada
zao kubwa za kuleta amani katika nchi hiyo.
Mwalimu
Nyerere ametunukiwa Tuzo hiyo inayoitwa 'Order of the National Republic of Burundi', kwenye Kilele cha
Sherehe za Kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Burundi
zizolifanyika leo, Independence
Road, pembeni mwa Uwanja wa Michezo wa Louis
Rwagasore mjini Bujumbura
na kutangazwa hadharani kwa maelfu kwa maelfu ya watu waliohudhuria sherehe
hizo.
Tuzo
hiyo ya Mwalimu imepokelewa kwa niaba yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mmoja wa viongozi sita wa nchi
za nje waliohudhuria sherehe hizo.
Akitangaza
Tuzo hilo, Rais wa Burundi, Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza alisema kuwa Burundi
imeamua kumtunuku Mwalimu Nyerere sababu mbili – moja ni ushauri wake muhimu
sana katika kuleta uhuru wa Burundi kutoka kwa wakoloni wa Kibelgiji.
Pamoja
na Hayati Mwalimu, aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela pia
amepata tuzo hiyo. Mzee Mandela alichukua nafasi ya Mwalimu kama mpatanishi wa
mgogoro wa Burundi
kufuatia kifo cha Mwalimu mwaka 1999.
Katika
sherehe hizo, zilizoendelea mfululizo kwa saa saba unusu tokea saa nne asubuhi
hadi saa 11 jioni, Rais Kikwete aliungana na viongozi wenzake wa nchi sita na
wawakilishi wa nchi nyingine nyingi duniani kuhudhuria kilele cha sherehe za
kufana kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Burundi.
Burundi ilipata uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kibelgiji
Julai 2, mwaka 1962 na Rais Kikwete aliwasili Bujumbura
asubuhi ya jana, akitokea Kigali, Rwanda, ambako pia alihudhuria sherehe kama hizo
Kuadhimisha Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Rwanda iliyopata uhuru Julai Mosi,
1962, kutoka kwa wakoloni hao hao wa Kibelgiji.
Tofauti
na Rwanda ambako Rais Kikwete alikuwa rais pekee aliyehudhuria sherehe za uhuru
wa nchi hiyo na mgeni rasmi, katika sherehe za Burundi, Mheshimiwa Rais na Mama
Salma Kikwete wameungana na Rais mwenyeji Pierre Nkurunzinza, Rais Mwai Kibaki
wa Kenya, Rais Theodore Obing Nguema wa Equatorial Guinea, Rais Joseph Kabila
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya
Afrika ya Kati na Rais Shariff Sheikh Ahmed Shariff katika kusherehekea uhuru
wa Burundi.
Walikuwepo
wawakilishi wa nchi nyingine nyingi duniani akiwamo Makamu wa Rais wa
Uganda na Makamu wa Rais wa Nigeria, Mheshimiwa Prince Philip ambaye ni
mtoto wa Malkia wa Belgium,
Waziri Mkuu wa Swaziland
na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) anayemaliza muda
wake,
Mheshimiwa Jean Ping.
No comments:
Post a Comment