• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, June 19, 2012

    Wema Sepetu kumleta nyota wa kike wa Nollywood



    Bila shaka wewe ni mmoja wa watu wenye maswali mengi kuhusu maana ya tangazo linalopigwa sana redioni na linaloishia tu kutaja jina la Wema Sepetu! What the hell is going on? Ni swali la kila mmoja hili.
    Well, hiyo ni ‘teaser’ ya kitu kikubwa ambacho Wema atakifanya mwezi huu jijini Dar es Salaam.
     Mchumba huyo wa zamani wa Diamond na former Miss Tanzania (2006) anatarajia kumleta nyota wa filamu wa Nigeria, mwanadada Omotola Jalade.
    Ujio wa Omotola nchini uliofanyiwa makeke na Wema umetokana na dhamira ya mlimbwende huyo mwenye sauti nyembamba kama mtoto wa miaka kumi na ushee, kuipeleka Bongo film industry to whole another level!
    Wema atafanya uzinduzi wa filamu yake mpya iitwayo Super Star, tarehe 23 mwezi huu.
    Katika filamu hiyo Wema, ameamua kuonesha safari yake ya kufikia usupastaa alionao leo kuanzia utotoni, kushiriki kwake Miss Dar Indian Ocean, Miss Kinondoni, Miss Tanzania hadi kuingia kwenye filamu.
    Omotola anatarajia kuikanyaga ardhi ya Tanzania wiki hii.

    No comments:

    3500K