"Simjui huyo Ney ni nani anaigiza
filamu au ni demu gani? mimi najua majina kama hayo ni ya mademu sasa
iweje Neema anidiss mimi?"
NI
kauli ya nyota mwenye 'Crown' ya mkali wa Rhymes nchini Seleman Msindi
'Afande Sele' alipokuwa akizungumza na Teentz.com kuhusiana na 'diss'
dhidi yake iliyotolewa na msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuchana hivi
sasa hapa Bongo, Ney wa Mitego kupitia track yake mpya iliyopewa jina
la 'Nasema Nao'.
Akizungumza na
mtandao huu namba moja ka habari za mastaa, Afande Sele mwenye maskani
yake pande za Morogoro amesema kuwa kamwe hajawahi kusikia wala
kujua kama kuna msanii wa hip hop hapa Bongo anayeitwa Ney na
kusisisitiza kuwa hamjui huyo mtu kabisa.
Alipotakiwa
kusema kama ameisikia Track hiyo Sele alifunguka kuwa hajui kitu
chochote kuhusu wimbo huo na anaamini kuwa hakuna wimbo wa Hip hop
ulitolewa hivi karibuni.
"Binafsi
sijaisikia na sijui lolote,nitajaribu kufuatilia,nitaitafuta track hiyo
niisikilize na kama atakuwa amefanya hivyo basi nitamlinganisha na mtu
anayemtukana Usain Bolt halafu akaanza kukimbia alisema Sele.
No comments:
Post a Comment