JUNI 15, mwaka huu, wapenzi zilipendwa, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Wema Isaac Sepetu wanatarajiwa kukutana uso kwa uso kwenye shindano la kumsaka Miss Dar City Center 2012 ndani ya Hoteli ya Golden Tulip, Masaki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, msemaji wa Kampuni ya Allure Internatonal inayoratibu ‘iventi’ hiyo, Martin Kadinda alisema kuwa Wema atakuwa ni jaji wa shindano hilo huku Diamond akiwa mburudishaji atakayeangusha shoo ya kihistoria.
“Kwa vyovyote lazima watakutana tu kwani hakuna namna ya kukwepana. Mashabiki wao waje kwa wingi wakawashuhudie laivu. Tiketi zinapatikana Shear Illusion pale Mlimani City na kwa maelezo zaidi watembelee blogu ya 8020fasions,” alisema Martin.
No comments:
Post a Comment