HUKU sakata la mirathi ya marehemu Steven Charles Kanumba aliyekuwa
gwiji wa filamu Bongo, likiendelea kufukuta chini kwa chini, baba mzazi
mzee Charles Kusekwa Kanumba amegawanya mali za mwanaye, Risasi
Mchanganyiko linakufunulia.
Mali za marehemu Kanumba zinazotajwa katika mgawo huo ni pamoja na
kampuni yake iitwayo Kanumba The Great Film Company na magari.
HABARI KAMILI
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka Shinyanga, mzee
Kusekwa (pichani) alisema yeye kama baba wa marehemu ana jukumu la kuwa
msimamizi wa mirathi na kugawa mali za mwanaye.
“Tumekaa huku Shinyanga na ndugu wengine, hili suala la mirathi
linapaswa kuwa chini yangu kwa sababu mimi ndiye baba. Kimila za kikwetu
(Kisukuma), msimamizi wa mirathi huwa ni baba,” alisema mzee Kusekwa.
Akaongoza: “Kutokana na hilo, nimechukua jukumu la kugawa mali za
marehemu mwanangu kwa kuzingatia usawa, haki na vigezo muhimu.”
MGAWANYO WENYEWE
Katika mgawo huo, mzee Kusekwa alitaja sehemu za mali za marehemu Kanumba huku akiacha nyingine.
Mali ambazo hakuzitaja na zinajulikana ni pamoja na akaunti za benki,
viwanja viwili vilivyopo Mbezi, Msakuzi nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam pamoja na mali nyingine.
Aliwataja mama mzazi wa marehemu, Flora Mtegoa, mdogo wa Kanumba
aliyekuwa akifanya naye kazi kwa karibu enzi za uhai wake, Seth Bosco.
Alisema, katika mgawo huo yeye kama baba anastahili kuchukua gari la
kifahari alilokuwa akitumia mwanaye wakati wa uhai wake, aina ya Toyota
Lexus na Bi. Mtegoa achukue gari ndogo aina ya Toyota GX 110.
“Ile kampuni ya filamu (Kanumba The Great Film Company) watachukua Seth na dada yake,” alisema mzee Kusekwa.
Kwa sasa, wanaosimamia kampuni hiyo iliyopo Sinza, Mori, jirani na Baa
ya Meeda jijini Dar es Salaam ni Seth na dada yake aitwaye Bela.
MPANGO WAKWAMA
Wakati hayo yakiendelea, ilielezwa kuwa mzazi huyo alituma wawakilishi
wake kutoka Shinyanga hadi jijini Dar kwa lengo la kufungua mirathi.
Habari za ndani kutoka kwa chanzo chetu makini ambacho hakikupenda jina
litajwe gazetini, zinasema kwamba wawakilishi hao walifika katika
Mahakama ya Mwanzo ya Kinondoni lakini walikwama.
“Hawafanikiwa kufungua mirathi maana hawakuwa na vielelezo vya kutosha.
Walitakiwa kuwa na cheti cha kuzaliwa na cha kifo cha Kanumba pamoja na
vielelezo vingine ambavyo hawakuwa navyo,” kilisema chanzo hicho na
kuongeza:
“Basi baada ya kukwama, hawakuwa na la kufanya zaidi ya kurudi Shinyanga.”
MAMA KANUMBA
Mama wa marehemu Kanumba, Bi. Mtegoa alipoulizwa anachofahamu kuhusu
ujio wa wawakilishi wa mzazi mwenzake alisema: “Nilisikia wamekuja,
lakini sijapata kuwaona kabisa. Tumesubiri mpaka sasa kuona kama
tutaitwa mahakamani lakini hatujaitwa.”
Akaongeza: “Kiukweli sijui nini kimetokea, maana siku chache baada ya
arobaini ya mwanangu, tuliweka kikao hapa Dar na mwenzangu (baba
Kanumba) alituma watu wawili waliokuja kumuwakilisha.
“Baada ya makubaliano hayo, tuliwekeana sahihi wanandugu wa pande zote
mbili na hata baba Kanumba alikubaliana na watoto wake waliokuja
kumuwakilisha kuhusu uteuzi huo...sasa haya tena yananishangaza maana
hata mahakamani kufungua mirathi bado sijaenda.”
Source
Saturday, June 9, 2012
Home
Unlabelled
Mali za Kanumba Za Kawanywa Kama Ifuatavyo
No comments:
Post a Comment