• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, June 21, 2012

    Wastara Ashukuru Watanzania-"Baada ya Miezi Mitatu Sajuki Anaweza Kuanza Kuigiza"



    Maombi ya watanzania pamoja na michango yao ya fedha vimesaidia kumfikisha mwigizaji Sajuki hapa alipo baada ya kupata nafuu kubwa toka apelekwe India kuitibiwa.

    Wastara akizungumza exclusive na millardayo.com amesema Sajuki anaweza kuanza kuigiza hata sasa kwa sababu nguvu imesharudi, anaweza kutembea kwa muda mrefu na hata hali yake ya sasa imebadilika sana tofauti na mwanzo.

    Amesema “baada ya miezi mitatu Sajuki anaweza kuanza kuigiza kama yeye mwenyewe atapenda na hata sasa hivi alipo pale unaweza kwenda nae location hana wasiwasi wowote ila kwa sababu ni mtu amefanyiwa upasuaji anahitaji kupumzika zaidi huwezi kutoka nae kwa sababu kuigiza inahitaji akili zaidi lakini baada ya miezi mitatu anaweza kuendelea na kazi”
    kwenye sentensi nyingine Wastara amesema hawezi kuzuia Sajuki kupigwa picha za Tv na magazeti kwa sababu kupitia vyombo hivyo vya habari ndio walifahamu kwamba anaumwa na wakaamua kumchangia sasa ni lazima wajue pia anaendeleaje kupitia vyombo hivyo hivyo na sio kwamba anamdhalilisha

    No comments:

    3500K