• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, June 21, 2012

    Kila saa moja Shetta alilipa laki na nusu Golden Tulip kushoot video ya ‘Nidanganye’



    Shetta alitaka kufanya kitu tofauti mwaka huu. Baada ya kukutana na pacha wake Diamond (kama wanavyojiita wenyewe) na kufanya ngoma iitwayo ‘Nidanganye,’ aliamua kufanya video kwenye hoteli ya kiima cha juu kidogo.
    Katika kuchagua mahala pa kufanya, uamuzi ulifikiwa kuwa video hiyo ifanyike katika hoteli ya Golden Tulip. Huwezi amini walicholipa kila baada ya saa ya shughuli nzima ya kushoot video hiyo chini ya super director Adam Juma wa Visual Lab; Next Level!
    “Tulifanyia location pale Golden Tulip. Kila baada ya lisaa tulikuwa tunalipa laki moja na nusu na video yote imefanyika pale. Plus room, room ni dola 350 pale. Nakumbuka tulianza saa kumi jioni tulitoka pale saa tisa usiku ama saa kumi kasoro,” Shetta ameiambia Bongo5.
    Hivyo ukijumlisha na gharama zingine kama za mavazi, kumlipa Adam, usafiri na mambo mengine video hiyo imemgharimu shilingi milioni 5.
    Good news kwake ni kuwa gharama hiyo tayari imesharudi na sasa anapiga faida tu, muziki unalipa!
    “Yeah ofcousre, sababu show moja milioni mbili, milioni mbili na nusu, hamna hamna moja nane kwahiyo isharudi.”

    No comments:

    3500K