Kama unadhani kuwa nyimbo za Nigeria zina umaarufu nchini kuliko
nyimbo za Tanzania zinavyojulikana nchini Nigeria, unaweza kuwa wrong!
Ngoma ya Alikiba– Single Boy inabang kinoma nchini Nigeria.
Infact kituo cha radio kinachosikilizwa zaidi kwenye mji mkuu wa
kibiashara nchini Nigeria, Lagos, The Beat 99.9 FM kimeuingiza wimbo
huo kwenye chart zake.
Wiki hii radio hiyo kupitia ukurasa wake imetweet. “ #AfricanTop10
At number 3, we have “Single Boy” Ft. Lady Jay Dee (@JideJaydee) – Ali
Kiba (@AlikibaTZ4Real).”
Kwa taarifa yako tu ni kuwa Beat 99.9 FM – Lagos #1 Hit Music
Station! inasikilizwa na asilimia 49 ya ya wakazi wa Lagos wanaofikia
milioni 15.
Kwenye page yake ya Facebook ina zaidi ya mashabiki 300,000 na
Twitter ina zaidi ya followers 21,600. Hivyo kwa resume hiyo, hii si
radio ndogo.
Katika hatua nyingine jana kupitia Twitter, Alikiba amesema yuko
mbioni kuachia ngoma nyingine, “Get ready for my new track .its a sexy
song in another feelings.”
Monday, June 11, 2012
Home
Unlabelled
Single Boy ya Alikiba: Namba tatu kwenye radio maarufu ya Lagos
No comments:
Post a Comment