Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia
Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia (The Scorpions)
iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh.
124,038,000.
Mapato hayo yametokana na washabiki
31,122 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000,
sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Washabiki 25,901 walikata
tiketi za sh. 3,000.
Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni
sh. 18,921,050.85 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati
gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 6,555,000), bonasi kwa Taifa Stars
(sh. 15,767,542.37), waamuzi (sh. 13,372,000), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000),
maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing
Construction (sh. 2,000,000), umeme (sh. 300,000) na mafuta ya jenereta (sh.
200,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya
gharama za mechi ni sh. 12,834,481, asilimia 10 ya uwanja sh. 6,417,241,
asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 3,208,620, asilimia
20 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 12,834,481 na asilimia 45
ya TFF (sh. 28,877,583).
No comments:
Post a Comment