SIRI imefichukua kuwa madai kwamba ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb
Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ ni memba wa jamii ya siri inayodaiwa
kumwabudu shetani, Freemason a.k.a Wajenzi Huru zilianza kitambo lakini
sasa zimeshika kasi baada ya kunaswa kwa picha inayomuonesha
akisalimiana na mtasha kwa ishara ya Kifreemason, Ijumaa Wikienda
linaibumburua.
Kwa mujibu picha hiyo, tukio hilo lilijiri nchini Uingereza, mwaka jana, Diamond alipokwenda huko kwa ajili ya shoo.
MAVAZI
Ilidaiwa pia kuwa mavazi ya Diamond
(meusi) yalishabihiana sawia na yale ya mtasha huyo yanayoelezwa kuwa
sehemu ya mavazi ya jamii ya Freemason.
ISHARA
Kingine kilichoibua maswali ni ishara ya
salamu ya wawili hao ambayo ilitengeneza nembo ya Freemason ya ‘V’ au
bikari kwa namna walivyogusana kwa vidole.
Kwa mujibu wa wadau
walioiona picha hiyo iliyonaswa kwenye mtandao wa Twitter, Diamond
amekuwa na ishara nyingine nyingi za aina hiyo hivyo kuzidi kuzua utata
kama ni memba wa jamii hiyo.
“Lakini inawezekana kwa sababu nasikia
ukishajiunga unapata mafanikio ya ghafla. ‘So’ kuhusu hili, sina upande
wa kusimamia,” ilisomeka sehemu ya maoni kwenye mtandao huo baada ya
kuibuka mjadala mzito juu ya ishu hiyo inayozidi kushika kasi mithili
ya moto wa kifuu.
“Tungeshukuru kama Diamond mwenyewe angejitokeza
aseme ukweli kwani akinyamaza anazidi kutuweka njia panda,” ilisomeka
sehemu nyingine ya maoni hayo huku ikiungwa mkono na wengi.
UNATAKA KUMSIKIA DIAMOND? SOMA HAPA
Ili
kumaliza utata wa je, Diamond ni Freemason au la, Ijumaa Wikienda
lilibeba jukumu la kumtafuta ili aanike ukweli wake ambapo alikuwa na
haya ya kusema:
“Unajua mwanzoni nilikuwa sikumbuki ni lini na wapi
nilipiga picha ya dizaini hiyo. ‘Anyway’, isiwe kesi, nakumbuka ilikuwa
Uingereza kipindi kile nilikuwa na shoo nchini humo.
“Nakumbuka walinifuata watasha wengi tofauti lakini huyo mmoja alining’ang’ania sana nipige naye picha.
“Kwa kweli alinilazimisha sana kwa sababu mwanzo nilikataa lakini baadaye nikaona isiwe ishu nikampa ushirikiano alioutaka.
“Mimi sikuona matatizo alivyotaka tusalimiane kwa kugusisha vidole kwa
sababu nilikuwa sijui chochote kuhusu Freemason. Nimeijua baada ya
mambo haya kuyasikia kwa sana hivi karibuni.
“Kwa hiyo inawezekana siku hiyo waliniunganisha bila mimi kujua (kicheko).”
SASA UKWELI NI UPI?
Mara kadhaa Diamond amekuwa
akihusishwa na Freemason kutokana na mafanikio ya ghafla aliyoyapata na
mvuto alionao kwa mashabiki wake ndani na nje ya Bongo.
Ijumaa Wikienda lilipotaka kupata ukweli kutoka kwake, Diamond alifunguka:
“Si kweli bwana, mimi nazisikia tu hizi habari kama wengine. Nasikia tu
ipo hapa Bongo na kiongozi wake ni Sir Andy Chande, zaidi ya hapo sijui
chochote.
“Mimi ni mtu wa swala tano na mafanikio yangu naamini Mungu ndiyo kila kitu.”
KUNA MSANII MWINGINE
Mbali na mwigizaji
Jacqueline Wolper na marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ ambao
wamekuwa wakitajwatajwa na mambo ya Ufreemason, Ijumaa Wikienda
limetajiwa msanii mwingine ambaye yupo mbioni kujiunga akidai anakwenda
kufuata utajiri.
Monday, June 11, 2012
Home
Unlabelled
Soma Habari Inayo Muhusisha Diamond na Amani Za Ki Freemanson
No comments:
Post a Comment