Salum Kinje |
Taarifa rasmi za uhakika kutoka ndani
ya uongozi na kamati ya ufundi ya klabu ya Simba ni kwamba timu hiyo
imefanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji bora wa nafasi ya kiungo
kwenye ligi kuu ya soka nchini Kenya, Salum Kinje ambaye anaichezea AFC
Leopards.
Nikiwa na Salum Kinje nilipotembelea Kenya mwezi uliopita. |
Kinje ambaye ni mtanzania amesajiliwa
na Simba kwa kiasi cha fedha ambacho hakijawekwa wazi na pande zote
mbili, lakini amesaini mkataba wa kuitumikia Simba kwa miaka 2 na siku
chache zijazo ataanza mazoezi na timu yake mpya inayojiandaa kushiriki
michuano ya Kagame Cup inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment