Taarifa za kutatanisha zimeibuka
kuhusu afya ya Hosni Mubarak aliyeondolewa madarakani kufuatia
maandamano ya kutaka mageuzi nchini Misri mwaka jana.
Baadhi ya vyombo vya habari vimetangaza kuwa
uhai wake unasitiriwa kwa kutumia mashine baada ya kuhamishwa kutoka
gerezani hadi kwenye hospitali ya kijeshi mjini Cairo.Kiongozi huyo aliondolewa mamlakani mwaka jana kufuatia maandamano ya raia wa nchi hiyo yakupinga utawala wake.
Mwezi uliopita alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuamrisha mauaji ya baadhi ya waandamanaji hao.
Mara kadhaa kumekuwepo na taarifa za kutatanisha kuhusu afya ya rais huyo wa zamani lakini kila mara zimepuuzwa.
Taarifa hizo kuhusu afya yake zimetokea wakati ambapo maelfu ya waandamanaji wamekusanyika kwenye bustani ya Tahrir kulaani uamuzi wa baraza la kijeshi wa kujilimbikizia mamlaka.
Maandamano hayo yamepangwa na viongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood. Mgombea wa kundi hilo wa kiti cha urais Mohammed Musri anadai kushinda uchaguzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Lakini pia mpinzani wake ambaye pia alikuwa waziri mkuu chini ya utawala wa Rais Mubarak, Ahmed Shafiq naye anadai ushindi.
Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yatatanzagwa alhamisi.
Vuguvugu la Muslim Brotherhood limeahidi kumfungulia mashtaka mapya Hosni Mubarak punde tu litakapo pata madaraka na linataka ahukumiwe kifo.
No comments:
Post a Comment