Na. mwandishi wangu kutoka, Dodoma
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawasaka Watu
wawili kwa tuhuma za Unyang’anyi wa
kutumia nguvu baada ya kuwatisha kwa
jambia wasichana wawili raia wa Uholanzi na kisha
kuwapora vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni moja laki
mbili na sitini na nne elfu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Bw. ZELOTHE STEPHEN alisema Tukio hilo lilitokea muda wa saa saba na
dakika arobaini na tano mchana katika eneo
la area D Wilaya ya Dodoma Mjini, Karibu
na nyumba inayojengwa kwa ajili ya 0fisi na Makazi ya Mh. Waziri Mkuu
Bw. MIZENGO KAYANDA PETER PINDA.
Alitaja vitu vilivyoporwa
katiika tukio hilo kuwa ni Kamera ya digitali aina ya Canon, Simu mbili za
mkononi aina ya Nokia na Samsung, Begi la Mgongoni, Viatu vya wazi pea mbili
(Sandal) Taulo la Hostel, Sketi, Wallet na Pesa za kitanzania shilingi 40,000/=.
Aidha aliwataja Waathirika wa Unyang’anyi huo kuwa ni wa LISA D/O LEMEN
mwenye umri wa miaka (19) na FLEUR D/O EDITH SCHOLTEN Mwenye Umri wa miaka (17)
wote ni Raia wa Uholanzi ambao wako nchini kama waalimu wa shule ya msingi na sekondari ya Saint Germa
iliyoko jijini Arusha inayofundisha watoto ambao wazazi wao wamefungwa gerezani.
“Raia hao wa Uholanzi ambao
walikuja kutembea Mjini Dodoma wakitokea Arusha walifikia katika Hostel ya
Saint Maria ambayo wanaishi wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule za
kutwa za mjini Dodoma”:
Kamanda ZELOTHE STEPHEN
alisema kuwa wageni hao walioporwa vitu hivyo, baada ya kufika katika eneo hilo wakiwa
na mwenyeji wao aliyejulikana kwa jina la Sister PONSIAN PROTAS MATAKA miaka
(43) ambaye anaishi katika Hostel waliyofikia wageni hao ya Saint Maria ilyopo
eneo la Uhindini.
No comments:
Post a Comment