Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s
Original leo imetangaza rasmi kudhamini shindano la kumpata mrembo
atakewakilisha taifa katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka huu,
yanayojulikana kama “Miss World 2012.
Akizungumzia
Udhamini wa shindano hilo linalojulikana kama “Redd’s Miss World 2012”
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International ambao ndio waandaaji wa
mashindano ya urembo hapa nchini Bw. Hashim Lundenga alisema; Ninajua
wadau wengi wa tasnia ya urembo watastuka kuona mabadiliko haya, hii
inatokana na kubadilika kwa ratiba ya mashindano ya Miss World toka
mwezi wa December ilivyokuwa ikifanyika awali na sasa yatakuwa
yakifanyika mwezi Julai hivyo kuwa na tofauti kubwa na ratiba ya
mashindano yetu ya Redds Miss Tanzania ambayo huanza mwezi Mei na
kumalizika Septemba. Ili tusipoteze nafasi yetu ya kushiriki mwaka huu,
kamati ya Miss Tanzania kwa ridhaa ya Serikali, iliamua kufanya shindano
dogo “Mini competition” ambalo litatupatia mshindi atakae wakilisha
Taifa katika mshindano hayo makubwa Duniani. Warembo
10 wataingia kambini tarehe 13 hadi tarehe 17 June, na shindano
litafanyika siku ya Juma Mosi tarehe 16 June katika ukumbi mpya wenye
hadhi ya kimataifa wa 327 Club, uliopo Mikocheni. Mshindi atazawadiwa
pesa taslim shilingi Milioni mbili, na kupatiwa maandalizi yote kwa
ajili ya matayarisho ya safari yake kwenda kwenye mashindano ya Miss
World 2012 yatakayofanyika Inner Mongolia – China. Kutokana na umuhimu
wa kufanya shindano hili tuliwaomba wadhamini wakuu wa Miss Tanzania,
kinywaji cha Redds ili watuwezeshe kufanikisha mchakato huu, nao bila
kusita wakakubali. Hivyo tunawapongeza sana Redds kwa mchango wao mkubwa
katika tasnia ya Urembo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment