Wakazi
wa Eneo la Ukonga Majumba Sita Wilaya ya Ilala jijini Dar es sal;aam
jana walifunga barabara kuu ya Nyerere katika eneo hilo la majumba sita
kushinikiza kuwekwa kwa matuta katika eneo hilo kufuatia kukuthiri kwa
ajali za wakazi wa eneo hilo kugongwa wavukapo barabara hiyo.
Tukio
hilo lilitokea leo majira ya saa za asubuhi na kudumu hadi saa nane
mchana baada ya kijana mmoja kungongwa katika eneo hilo akijaribu kuvuka
barabara hiyo na kufa papo hapo.
Wakiwa
na mabango, mawe na matofali wakazi hao waname, wanawake, wazee kwa
watoto walifurika katika barabara hiyo na kushinikiza kuja kwa mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam na kuwekwa kwa matuta.
Wananchi
wakiwa wamefurika kwa wingi barabarani na hata Jeshi la polisi
lililopfika na kuwasihi waruhusu magari kupita waligoma na huko mitaani
pia walizuia boda boda (pikipiki) kupita hadi matuta yawekwe.
Magari yakiwa yamezuiwa eneo hilo karibu na Kambi ya Jeshi Kikosi cha Anga.
Wananchi wakiwa upande wa pili wa barabara kutaka kujua hatma ya usalama wao.
Watu
walikuwa ni wengi. Awali eneo lingine katikati ya Njia Panda segerea na
Minazi Mirefu (Banana) wanafunzi wa shule ya Msingi Minazi Mirefu
waliwahi kuandamana barabarani hapo kushinikiza kuwekwa kwa matuta baada
ya wenzao kadhaa kugongwa na serikali ikaweka matuta hayo na hivi sasa
hali ni shwari katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment