Meli hiyo inavyoonekana kwa Nje
Meli hiyo inavyoonekana kwa ndani.
Meli hiyo inavyoonekana kwa Ujumla
---- .
Azam yaamua kufanya kweli na hivi
karibuni meli ya kisasa iko mbioni kuzinduliwa ambayo ikawezesha watu
kwenda na magari yao Zanzibar. Meli hiyo inauwezo kubeba magari 200,
abiria 1500 na Mizigo tani 500.KAMPUNI
ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa
ya kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja.
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka
huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa.
Mohamedi alisema shida ya
usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na
uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo
abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es
Salaam ataweza kufanya hivyo.
Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.

No comments:
Post a Comment