Desemba
mwaka jana utakumbuka kuwa kuna mwandishi wa habari wa kujitegemea wa
kule mjini Iringa ndugu Godwin Francis alidai kupigwa na Msanii wa
muziki Diamond na kupeleka kesi hiyo kwenye mahakama moja huko Iringa
ambapo hakimu aliamuru mshitakiwa amlipe mlalamika kiasi cha kisichozidi
laki 2 licha ya mlalamikaji kudai milioni 30 juu ya kupigwa na
kuharibiwa mali zake. Lakini baada ya kesi hiyo Godwin alitoa siku 30
kwa Diamond ili aweze kumlipa hizo milioni 30 na endapo hatafamya hivyo
atafikisha kesi hiyo mbele zaidi ya sheria lakini Diamond hakufanya
hivyo. Lakini jana kupitia media
kadhaa waliweza kutoa habari kwamba Godwini yuko Dar
na wamekaa chini na Diamond kulimaliza tatizo hilo wakiwa chini ya
wapatanishi kadhaa na kudai kuwa swala hilo linaelekea kuisha, kama
unavyowaona pichani ni picha waliyopiga baad ya kupatanishwa.
Wednesday, June 20, 2012
Home
Unlabelled
ALIYEPIGWA MAKONDE NA DIAMOND NA KUHARIBIWA VITU VYAKE WAPATANISHWA!
No comments:
Post a Comment